Get free web hosting, free domain, free website/blog

Web hosting

Wednesday, October 12, 2016

UKWELI KUHUSU ALI KIBA KUZIMIWA MIC AKIWA JUKWAANI NCHINI KENYA NI HUU

Hivi juzi kati mnamo mwa tarehe wa 8 mwezi huu kulifanyika bonge la show moja la kufa mtu ambapo lilifanyika nchini kenya
Huku likijumuisha wasanii lukuki ambao wengine wana tikisa dunia kwa sasa
Kulikuwa wasanii kutoka nchi tofauti akiwemo chris brown kutoka Marekani
Wizkid kutoka Nigeria pia alikuwa vannesa mdee na pamoja ali kiba kutoka Tanzania
Chris Brown ni msanii mkubwa kutoka marekani ambae anatikisa Afrika na ulimwengu kwa ujumla msanii huyu ngali kutoka marekani anatikisa kibao kama new flame, paradise, grass ain't greener, without you, with you, zero, liquor, na nyingine nyingi ambapo kwa hivi kibao kinacho wateka mashabiki zaidi grass ain't greener.
Wizkid ni msanii nyota kutoka Nigeria ambapo wiki kadhaa zilizo alikuwepo Tanzania kwa ajili show ya fiesta 2016 iliyo fanyika jijini mwanza na mashabiki wa mwanza waliinjoi show hiyo kwa kweli
Pia wizkid anatamba vibao vyaka kama azonto, show you my money, holla at your boy, in my bed, lakini kwa hivi wizkid anatikisa na kibao chake cha kukata na shoka kile cha final (baba nlai).
Tukija kwa vannesa mdee kama ijulikanavyo vannesa mdee ni msanii mzurii kutoka Tanzania na anafanya vizuri kwnye soko la mziki wa bongo na Afrika na dunia kwa ujumla pia vannesa anatamba na vibao vyake nguli kama closer, nobody but me, niloge, comer over, never ever pia vannesa mdee anatikisa kibao chake cha juu ambacho kamshrikisha mpenzi wake juma jux.
Tukija kwa ali kiba kama ijulikane ali kiba ni msanii mwenye washabiki wengi sana Tanzania pamoja na East Afrika huku star huyo akizidi kushika kasi baada ya kutoa kibao chake cha aje ambapo ndio kinatikisa kwa hivi sasa na kama ijulikanavyo ali kiba ana mvutano mkubwa wa kimuziki ambae pia nguli katika soko la muziki ambae ni diamond platnumz.
Licha ya show hiyo iliyo fanyika mombasa nchini Kenya kuwa show iliyo vunja rekodi kwa kuingiza mapato mengi kwa kuudhuliwa na watu wengi kuliko kawaida lakini kilitokea kituko cha mwaka ambapo ilipo fika zamu ya msanii kutoka Tanzania ambae ni ali kiba ambapo alipo panda tu jukwaani na kuimba nyimbo mbili ,tatu gafla alizimiwa maiki katika hali ya ya sinto fahamu na kumfanya ali kiba kushuka huku akiwa kicha chini na kupandishwa chris brown kutoka marekani.
Baada ya tukio kumkuta ali kiba alisikika akisema nanukuu "nilimuona boss wake na diamond sallam back stage kipindi nashuka kwa maana hiyo sallam alikuw back stage kipindi mimi napafomu lakini najiuliza mwenyewe sallam alifwata nini back stage kipindi mimi napafomu na ikiwa na ina fahamika mimi na wao hatuna maelewano mazuri unadhani watu watachukuliaje yeye kukaa back stage ikiwa mimi napafomu yeye ni nani mpaka akae back stage yangu kama angetaka kuangalia show si angekaa V.I.P aangalie show kwa nini aje back stage" mwisho wa kunukuuu
Ali kiba alisikika akisema haya kwenye kipind cha mambo mseto ambacho kinarushwa na chanel ya citizen
Kwa maana hiyo basi ali kiba anaamini sallam kukaa back stage wakati yeye ana perform ni moja ya sababu iliyo mpelekea yeye kuzimiwa maiki
Lakini ukweli kuhusu ni huu hapa show ilianza usiku mida ya saa moja ambapo baada ya wasanii kadhaa kutoka nchini kenya kutimbuiza ilitakiwa apande vannesa mdee akifwatiawa na ali kiba alafu na wizkid alafu mwisho alitakiwa mzee mzima Chris Brown apande ili kufunga show hali ya taharuki ilitokea ambapo ilipo fika zamu ya ali kiba alisubiriwa takribani dakika 30 nzima kupanda jukwaani lakini ali kiba hakutokea jukwaan na ndipo ratiba ikaamua kubadilishwa akapanda wizkid badala ya ali kiba akapafomu na alipo maliza ndipo ali kiba ali kando mwa jukwaa na ndipo akapanda yeye lakin kituko cha mwaka kilitokea pale ali kiba alipo panda nakuanza kupiga show dakika kadhaa baada ya show gafla alizimiwa mic au kipaza huku sababu ikiwa haijulikani ni nini
Mwandamizi wa show anasema ali kiba alitumia mda mwingi kwenye kujiandaa hvyo kumpelekea mpka kuchelew kupanda jukwaani na wakaamua kumpndisha wizkid badala yake
Lakini pindi ali kiba alipo kuwa yupo jukwaani mda wa chri brown ulikuwa umefika kwa ajili ya kuperform hivyo walishindwa kumshusha ali kiba jukwaani kama mbwa kwani ni msanii mkubwa pia East Africa na Africa kwa jumla na badala yake walimuamulu dj kuzima mic (kipaza sauti) ili ali kiba ashuke na apande Chris Brown
Taarifa zinasema Chris Brown akuwa akuwa na mda wa kupoteza kwani alikuwa anatakiwa aondoke na ndege ya saa 9 usiku siku hiyo hiyo kwa hiyo kama wangeli endelea kumuweka ali kiba jukwaan basii wange mchelewesha Chris Brown na baadae inge wagarimu pesa nyingi kumkodishia ndege nyingine kurudi kwao marekani