Get free web hosting, free domain, free website/blog

Web hosting

Thursday, September 22, 2016

(Official lyrics) Diamond Platnumz Feat Raymond- Salome (na maana yake)


DESCRIPTION:

Song: Salome

Artists: Diamond Platnumz Feat Ray Vanny

Originated From: Maria From: Saida Karoli

Label: Wasafi Classic Baby(WCB).

Country: TANZANIA

Video By: NicorouxFrom: South Africa

Written By: Diamond Platinumz&Ray Vanny.


Produced By: Lizer Classic

Released: September 18th 2016

Video made: 10th April 2016.

Video Location: Dar Es Salaam, Tanzania.

Video Queen: Hamisa Mobeto.

Contacts: +255713700400 +255715333346 Email: Diamondplatnumz@gmail.com sallam.sharaff@gmail.com babutale44@gmail.com

Buy On Itunes: https://geo.itunes.apple.com/us/album...

Stream On Spotify: http://open.spotify.com/album/2HvsOe6...

Stream On Youtube: https://youtu.be/_bPjsDcPHks

Follow Diamond Platnumz On Social Medias: twitter: @diamondplatnumz Facebook page: https://www.facebook.com/DiamondPlatn... Follow on G+: https://www.google.com/+TheDiamondpla... Follow on Instagram: http://www.instagram.com/diamondplatnumz

LYRICS

[Intro]

WASAFIIII

[Verse – 1 by:Raymond]

Kioo hakidanganyi mamaa, umejipodoa umepodoka.

Mwendo na shepu vyote mwanana, Mimi suruari yanidondoka,

Tukimbizane nini salome wangu? Iyo michezo ya jogoo,

Mbona watizama chini salome wangu Ukimuona jongoo,

Inama kidogo shika magoti Nimesimama kama ngongoti,

Mtoto jojo sio roboti Chumbani bingili bingili sambasoti.

[Chorus By: Diamond]

Unanitekenyaga ukinyonga salome, (Unanitekenyaga ukinyonga)

Unatikenyaga ukinyonga kweli, (Unanitekenyaga ukinyonga, Aaaha!)

Hoera makulu vane, hoera ngambe

Hoera na Zari, hoera ngambe

[[Verse – 2 By: Diamond Platinumz]

Utamu kolea aprokoto, Ting’ari ting’ari ndani kwa moto Nitamnyongea, msokoto.

Niteme sumu kali kama koboko

Eeeh Mapenzi yananipa shida, Shida maama,

Ni donda lisilokuwa na tiba,Tiba bwana.

Usije baby kanicharanga, Kanichambua moyo kama karanga.

Mie baby kwenye msambwanda, huwa siendagi ngenge ni nganganga.

[Chorus By: Diamond PLatnumz]

Unanitekenyaga ukinyonga salome, (Unanitekenyaga ukinyonga)

Unatikenyaga ukinyonga kweli, (Unanitekenyaga ukinyonga, Aaaha!)

Hoera makulu vane, hoera ngambe

Hoera na Zari, hoera ngambe

[Verse-03 By: Ray Vanny]

Uhm yeeh, Mwenzako nyang'anyang'a, Uhm mie binzari we ndo nyanya.

Baby kwang'aru, Nisimamie kama kangaruu.

Ibane kangwaru,Babu Juma mupige kwakwaru.

(Kwakwarukaa eeeenh)


[Bridge By: Diamond Platinumz]

Hasa chambua kama karanga sasa, (Chambua kama karanga)

Ichambue kama karanga Salome, (Chambua kama karanga)

Hasa washa, washa

Moto washa, washa

Songa, Songa

Ugali Song, songa

mpaka chini, haa chini

mpaka chini, haa chini

Wenye wivu wajinyonge leo, (wenye wivu wajinyongee)

Wenye wivu wajinyonge sasa, (wenye wivu wajinyongee)

Wenye wivu wajinyonge kweli, (wenye wivu wajinyongee)

oonh, Wenye wivu wajinyonge sasa, (wenye wivu wajinyongee)

Wanakodoa kodo,wanakodoa (macho kodo)

Wanakodoa kodo,wanakodoa (wale kodo)

Wanakodoa kodo,wanakodoa (ukinyonga)

Wanakodoa kodo,wanakodoa (Aa ukisonga)

Wanakodoa kodo,wanakodoa.

Asante kwa kupitia ukurasa wetu ya Mtukutu, na karibia tena kwa mara nyingine. ningependa kujibu yale maswali ambayo huwasumbuaga mashabiki wengi ndani ya Afrika Ya Mashariki kuhusiana na wimbo huu pamoja na video hii kwa kupitia historia fupi ifuatayo ya kuhusu wimbo huu......

Historia fupi kuhusu wimbo huu.

Salome ni wimbo wa mapenzi ulioimbwa kwa lugha ya kiswahili na kihaya(lugha inayopatikana kaskazini mwa Tanzania pamoja na kusini mwa Uganda) kwa mbali, wimbo huu uliimbwa na wasanii wawili maarufu kutoka nchini Tanzania waitwao "Diamond Platnumz" na "Ray Vanny" ikiwa na vionjo vya asili kutoka katika kabila la kihaya na ulitengenezwa kwa kutumia vionjo vinavyopatikana katika wimbo wa kihaya kutoka kwa msanii wa kike wa KiTanzania mwenye asili ya Kihaya "Saida Karoli" katika wimbo wake uitwao "Maria"

.

Wazo la kutengeneza wimbo huu lilipatikana ndani ya studio ya Wasafi Records ndani ya Dar Es Salaam, Tanzania na lilitolewa na Diamond Platnumz na hivyo kuamua kuwasiliana na Saida Karoli kibiashara zaidi. Diamond na Saida wakawekeana makubaliano ya kumlipa asilimia 25 ya mapato ya wimbo huu Saida na asilimia 75 kwenda kwa kundi la WCB.

Lizer Classic, producer pendwa ndani ya Wasafi Records ndipo alipopatiwa kazi ya kutengeneza mdundo special kwa nyimbo, pamoja na kumix,kudesign,kumaster, kulevel vocal zitakazoingizwa. Diamond akamualika Raymond(Ray Vanny) kama msanii aliyeshirikishwa.

Lyrics za wimbo huu ziliandikwa kwa ushirikiano baina ya Diamond&Ray Vanny, huku mgawanyiko wa verse ukiwa tofauti kidogo. RAY VANNY akapatiwa verse ya kwanza na ya tatu, huku Diamond akiwa amechukua verse ya pili, chorus, na bridge. Lyrics ya wimbo huu imejikita zaidi kwenye pendo motomoto, tendo la ndoa, uzuri wa mwenzi wake. Lyrics hii imesimamia kweli zaidi jinsi mtu anapopagawisha na umbile, utundu,na mahaba ya mpenzi wake.

Location ya video ya wimbo huu ilikuwa nchini Tanzania, huku Fursa ya kutengeneza video ya wimbo hii ilimdondokea director mkubwa nchini South Africa na Nigeria lakini bado si maarufu nchini Tanzania na Afrika ya mashariki kwa ujumla, namzungumzia director mzawa wa South Afrika "Nicoroux", tumezoea kuona video nyingi za Wcb kufanya na GodFather kutoka South Afrika na location yake kuwa South Afrika huku video queens wakiwa ni light skin au wasichana weupe, kwanini ndani ya video hii location ni hapa hapa Tanzania, director mpya, na video queens ni wa hapa hapa nyumbani na ni weusi???? Wazo la kufanya video hii nyumbani ni kwaajili ya kuuenzi utamaduni wa hapanyumbani tukiwa nyumbani kwetu pia hapakuwa na hitaji kubwa la kutafuta location South Afrika japo ilikuwa inawezekana.... Pia wcb ilihitaji kubadilisha upepo na kujaribu kuwapa ugali madirector wengine wenye vipaji ili nao wapate fursa ya kujitangaza zaid nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla ndipo zari la mtende likamdondokea Nicoroux akiwa ni moja kati ya waongozaji wanaokuja juu katika tasnia hii ya music nchini South Afrika. Pia moja ya sababu ya kuwachukua video queens wa hapahapa nyumbani ni moja ya njia ya kuwapa fursa watu wa nyumbani ili nao waweze kutusua zaidi kimataifa. Wazo kuu juu ya scene, watu, n madhali ilikuwa niushirikiano mzuri uliokuwepo kipindi cha utengenezaji wa script baina ya Diamond na Nicoroux.

Watu waliopata nafasi ya kuuza sura katika video ya nyimbo hii ni pamoja na Diamond Platinumz, Hamisa Mobeto, Rich Mavoko, Ray Vanny, Asma Platnumz, Harmonize, Jackline Wolper, Aunt Ezekiel, Mosee Iyobo, Wasafi Classic Dancers, Jack Platnumz, Tunda, na wengine wengi. Swali ni moja, kwanini Hamisa Mobeto na sio Zari Hassani??? na hivi karibuni kupitia radio mbao ilisikika kwamba Hamisa Mobeto anatoka Baba Tiffah, au ndo walikuwa wapo katika utengenezaji wa hii video mwezi wa nne mwaka huu alafu team Zarimond wakazusha yao? au ni kweli kwamba wawili hawa wapo pamoja mana tumeona wengi katika video hii wakiwa na wapenzi wao wa ukweli, je hawa wawili nao vepee?? mh, hayo sio kazi yangu ila nikipata ubuyu zaidi nitakuja kukujuza juu ya hili.

Mapokeo ya nyimbo hii nimakubwa sana tena tofauti na yale ya wimbo uliopita "Diamond feat P-square: Kidogo" , watu wengi waonyesha kuridhishwa na kazi hii na kumpongeza Diamond&Ray Vanny kwa kazi bora isiyochosha akili. Kupitia mitandaon nyimbo hii imeweka record ya kuwa wimbo uliotazamwa zaidi kutoka sept 18th 2016 mpaka sasa huku ikijizolea views 3million kwa mda wa siku tatu. na pia kuwa most shared song ndani ya instagram huku fans tofauti wakionekana kupost vipande vya lyrics vya wimbo huu. pia ndugu pia hawapo nyuma, Asma Platinumz alimpongeza Diamond kwa kusema "Moja ya sababu inayofanyaga video za WCB ziwe nzuri na kutokana na yeye mwenyewe DIAMOND kuwa ndiye mastermind wa kila kitu kitakachofanyika. "

Asante kwa kuwa nami mwanzo mpaka mwisho wa habarin hii, natumaini nitakuwa nimeyajibu maswali yenu yaliyokuwa yakiwasumbua kuhusu nyimbo hii kwa asilimia 75, toa coment yako hapa chini au swali lako au kama una pendekezo, wazo, chaguo nasi tutakutimizia mahitaji yako kama yatakuwa ndani ya uwezo wetu. share na marafiki zako, na nakutakia siku njema yenye furaha. ASANTE.


11 comments:

  1. Ilove ur post, na nimevutiwa na uandishi wako pamoja na fact zako. asante kwa information na kumaliza maswali niliyokuwa nikijiuliza. mondi hii ngoma tamu sanaaaaaa.

    ReplyDelete
  2. Kazi nzuri, nmeitafuta hii lyrics mpaka nikachoka ila asante kwa kunisaidia kwa hilo. hii nyimbo nimeipenda sana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante sana ndugu, karibu tena na usipate shida sana we toa tu suggestion na sisi tutakutafutia na kuipost ontime.

      Delete
  3. Nyie watu mko makini sana na kazi yenu, hamjakosea hata kidogo. naipenda sana hii nyimbo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Karibu sana kaka, jisikie huru na uendelee kuburudika.

      Delete
  4. Thank u mtukutu, ila kuhusu mobeto kuwa ndo video queen mi nahisi kawekwa tu auze sura plus zile skendo labda zilikuwa zakumpa kick tu cunajua wcb wazee wa skendo. nice song btw.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yeah kweli hata mi hahisi hivyo hivyo. kutafutiana kick tu.

      Delete
  5. Wee mtukutu cuajiliwe tu kwenye gazet ndugu yangu ili tuwe tunapata data zilizojitosheleza kama hiz?, Zari ndo mama mjengo huyo Hamisa shobo tu, upo
    .

    ReplyDelete
  6. maanake halisi ya aya ya tatu? nyang'anyang'a, kangwaru, kwakwaru??

    mashairi yachachawiza kweli!

    ReplyDelete