Get free web hosting, free domain, free website/blog

Web hosting

Friday, September 16, 2016

Skendo ya Diamond,Zari na Huddah Monroe kuendelea kuvuma huku Wasafi Classic Kukinukisha ndan ya Burundi September 24, 2016

Kundi zima la Wasafi Classic Chini ya the big boss Diamond Platinumz pamoja na majembe yake matatu Harmonize, Ray Vanny, na Rich Mavoko wanatarajiwa kukinukisha ndani ya Burundi siku ya tarehe 24 mwezi 09 mwaka 2016 kwa show kali zitakazo tikisa miji yote ya Burundi.
diamond platinumz,ray vanny, harmonize na rich mavoko wakifanyiwa interview katika kituo cha radio.
(Kwenye picha ni kundi zima la WCB wakiwa katika kituo kimojawapo cha Radio hapa nchini.)

Kabla ya kuelekea Burundi tarehe 24, kundi hilo la Wasafi Classic lilipitia kutumbuiza nchini Kenya na kuacha historia iliyowafanya mashabiki wasisahau kuhusu show hiyo.
Diamond alipokelewa kwa shangwe la kutosha lilimfanya aone kama ni jambo kubwa la kihistoria katika maisha yake.
Lakini kuna tetesi tetesi zilizo enea mtaani kupitia radio mbao na blog za udaku za nchini Kenya kuhusu kitendo kilichotokea usiku wa siku ya show hiyo nchini Kenya ambacho kinasemekana kwamba ni nusu kihatarishe mapenzi baina ya Zari The Boss Lady na Diamond Platinumz, je ni kitendo kipi hicho??? Ngoja nikupe ubuyu.

Soma hapa (Na nukuu kutoka katika moja ya blog ya udaku kutoka nchini Kenya iitwayo TUKO.CO.KE ambayo nayo ilitoa taarifa hiyo.)
"ZARI HASSAN AMSHAMBULIA HUDDAH, BAADA YA HUDDAH KUMPATIA MAMBO MOTOMOTO DIAMOND PLATINUMZ KWA SIRI"

"Kumekuwa na maneno mengi yalizoua vitendawili katika vichwa vya mashabiki wengi kuwa Diamond Platnumz hakulala peke yake kipindi hichi alichotembelea Meru,Kenya kwaajili ya Tamasha.
- Vyanzo vya karibu vinasema kwamba mwanamziki huyo(Diamond Platnumz) alilala na rafiki kipenzi wa mke wake(Mama Tiffah) yani na maanisha Huddah Monroe, mfanyabiashara na mashuhuri kwa kujihusisha na mambo mengi ya kijamii nchini Kenya na Duniani kwa ujumla."

 Chanzo hicho kiliendelea kwa kusema kuwa, Huddah Monroe alimkaribisha kwa ukarimu mwanamziki huyo nchini Kenya kwa kuuendeleza urafiki wao wa kifamilia hadi kitandani, blog nyingi nchini Kenya na Tanzania zimekuwa zikiripoti skendo hii kubwa iliyozikuta familia hizi mbili maarufu ndani ya East Africa.
picha ya Diamond platnumz akila denda na huddah na kusababisha ugomvi na Zari.
(.Picha ya mwanadada Huddah Monroe, anayedaiwa kutoka na Diamond Platnumz.)

Kabla ya hayo yote kutokea, Huddah na Zari Hassan walikuwa ni marafiki wakubwa na imeripotiwa mara nyingi familia hizo wamekuwa wakialikana na kupata pamoja chakula cha ijioni ndani ya State House, Tegeta, Dar Es Salaam, Tanzania.
Na hata mwaka 2015 pale ambapo Zari alipotembelea Kenya kwa ajili ya Grand-All White Party ndani ya Skyluxx, alikuwa bega kwa bega na Huddah Monroe kuanzia maandalizi mpaka mwisho wa party hiyo.
Zari alianza kuingiwa na wasiwasi kuendana na mienendo ya rafiki yake huyo japo hakuwa na uhakika wa kile kinachofanyika nyuma ya pazia.

Wiki Iliyopita  mwanadada Zari The Boss Lady aliingia kwenye vita ya maneno na rafikiye Huddah Monroe kupitia mtandao wa Snapchat na kusababisha watu wengi kugundua tatizo lililopo kati yao na kuacha watu midomo wazi huku wengi wakiwa hawajafurahishwa na kitendo hicho alichokifanya Baba Tiffah cha kuwamix marafiki hao kwa tamaa za mwili wake.
Kila mmoja alikuwa akipost maneno makali kuhusu bwana wao huyo huku kila mmoja akimshambulia mwenzake kwamba yeye ndo mmiliki halali wa bwana huyo.
HUDDAH "“When you think your man is yours kumbe (yet) he is ours. And I ate and dined with both of you. Having kids with someone to tie him down doesn’t mean he won’t leave. The little boy is public property, you order him like pizza. Don’t hate the player or the game, hate yourself, Madam!” Huddah ranted on Snapchat.
 Naye Zari alijibu kombola hilo kwa kupost picha akiwa na mmewe Diamond Platnumz a.k.a Baba Tiffah kwa caption kaaali, check hapa.
“Watu na bae zetu… nyaku nyakus can’t even post their own. Told you, if he can’t claim you in public, don’t give him the goods in private. You know what that means right and I bet you know where that leaves you. Tag your bae and wish him or her a good night. #ToWhomItMayConcern.” Zari alipost status hiyo."
**********Mwisho Wa Kunukuu*********
Inaonyesha wazi kuwa marafiki hao si kitu tena, mana Zari hapendi urafiki wa kinafki.
na kama misemo ya wahenga isemavyo "Cheza na akili lakini usicheze na mpenzi wangu"
Diamond mpaka sasa bado hajaweka wazi kuhusu taarifa hizo na kama inavyojulikana kwamba Zari na Diamond ni baba yoyoo na mama yoyoo wa mtoto mmoja (princess Tiffah) na mwingine nusu ambaye bado yupo tumboni na anatarajiwa kuzaliwa hivi karibuni, sasa wewe Huddah vepee??? mbona wataka kutia chumvi kinyama cha watu???
Taarifa za kutoka kwa marafiki wakaribu wa Huddah zinasema kwamba Huddah ana mpenzi wake japokuwa amekuwa akipenda kuendelea kuonekana single na huwa hapendi kumuonesha mpenzi. mh, haya????!!!!!!

Ndugu Wasomaji tutaendelea kuwa-update kuhusu jambo hili mpaka tuujue mwisho wake. Karibu tena siku nyingine.
Umelichukuliaje jambo hili???? Hebu tupe feedback yako hapo chini kwa kutoa comment yako/mawazo yako.
na usisahau kusubscribe ili uwe unapata updates kupitia email yake kila siku.. karibu tena.

3 comments:

  1. Mondi anawachanganya tu kama zege. ningekuwa mi zari, ningemnyonga huyo Huddah.

    ReplyDelete
  2. Sasa je, brotha we wakate tu c wamejilengesha wenyewe.

    ReplyDelete
  3. Dah asante sana Mtukutu kwa huu ubuyu mana nilikuwa tayari nishapitwa. Huyu Mondi kazidi ndomana alitakiwa kubaki na Wema malaya mwenzie.

    ReplyDelete